Elizabeth II wa Uingereza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Elisabeth II mwaka 2006.

Elisabeth II ni malkia wa Uingereza (au Ufalme wa Muungano) tangu mwaka 1952. Katika historia yote ya dunia hakuna mtawala aliyedumu madarakani muda mrefu kuliko yeye.

Alizaliwa kwa jina la Elizabeth Alexandra Mary Windsor mjini London tarehe 21 Aprili 1926 kama mtoto wa kwanza wa mfalme George VI wa Uingereza na Elizabeth Bowes-Lyon.

Kama mkuu wa Jumuiya ya Madola yeye ni pia mkuu wa dola wa nchi zifuatazo ndani ya jumuiya hii:

Alitangazwa kuwa malkia tarehe 6 Februari 1952 mara moja baada ya kifo cha baba yake George VI. Wakati ule alikuwa akitembelea Kenya iliyokuwa bado koloni la Uingereza akatembelea milima ya Aberdare.

Alipokea taji katika ibada rasmi tarehe 2 Juni 1953 kwenye kanisa la Westminster Abbey.

Katika nchi zote anaposhika cheo hana mamlaka ya kiserikali anatawala kama mfalme wa kikatiba katika muundo wa serikali ya kibunge.

People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Elizabeth II wa Uingereza kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.