Twitter

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Logo ya sasa ya Twitter

Twitter ni mtandao wa kijamii unaotoa huduma ya kutuma vijiujumbe vidogo vinavyoitwa "Tweets" na kushea na watu wanaokufuata. Vilevle huduma hii hutazamiwa kama blogu ndogo. Watumiaji wanatumia simu za mkononi au kompyuta kutuma na kusoma jumbe. Tweet zinaweza kuwa na maneno yenye urefu wa 140 tu. Hata hivyo mwaka 2017 kampuni hii ilitangaza kuongeza idadi ya urefu wa maneno hadi 280.[1] Maneno haya au jumbe hizi zinaonekana katika ukurasa wa mtumiaji. Tweet hizi aghalabu zinaweza kusomwa na mtu yeyote, lakini mtumaji anaweza pia kuzifanya ziwe faragha. Tweet ambazo ni faragha zinaweza kuonekana kwa wale ambao wanakufuata tu.

Watumiaji wanaweza kujiandikisha na kutweet kwa watu wengine. Mtindo huo unaitwa following au kufuata, na wanaojiandikisha wanaitwa followers au wafuasi. Mwishoni mwa mwaka wa 2009, watumiaji waliweza kufuata orodha za muumbaji.[2][3]

Watumiaji wanaweza kupokea tweets kwa kutumia wavuti ya Twitter. Vilevile wanaweza kutumia programu pepe ambazo zinafanya kaza na Twitter kwenye simujanja. [4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Twitter will double its character count for most users.
  2. There's a List for That. blog.twitter.com (October 30, 2009). Iliwekwa mnamo February 1, 2010.
  3. Twitter Lists!. help.twitter.com (November 9, 2009). Iliwekwa mnamo February 1, 2010.
  4. Using Twitter With Your Phone. Twitter Support. Iliwekwa mnamo 2010-06-01. “We currently support 2-way (sending and receiving) Twitter SMS via short codes and 1-way (sending only) via long codes.”

Viungo Nje[hariri | hariri chanzo]